Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 5 · Aya ya 88

Al-Maaida 5:88

المائدة

وَكُلُوا۟ مِمَّا رَزَقَكُمُ ٱللَّهُ حَلَـٰلًا طَيِّبًا ۚ وَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ ٱلَّذِىٓ أَنتُم بِهِۦ مُؤْمِنُونَ

Maana

Na kuleni katika vile alivyowaruzuku Mwenyezi Mungu, vya halali na vizuri. Na mcheni Mwenyezi Mungu ambaye nyinyi mnamwamini.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na kuleni katika alivyo kuruzukuni Mwenyezi Mungu, halali na vizuri. Na mcheni Mwenyezi Mungu ambaye mnamuamini. [88]

[88] Na kuleni vitu alivyo kupeni Mwenyezi Mungu na akavifanya vyepesi kwenu, na akavifanya ni halali na ni vizuri kwa nafsi zenu. Na daima mwogopeni Mwenyezi Mungu, na mt'iini Yeye maadamu nyinyi mnamuamini Yeye.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na mstarehe, enyi Waumini, kwa halali nzuri Aliyowapa Allah Mtukufu na kuwatunukia. Na mcheni Allah Mtukufu kwa kufuata amri Zake na kujiepusha na makatazo Yake. Kwani kumuamini kwenu Allah Mtukufu kunawalazimisha nyinyi kumcha Yeye na kuwa makini(1).

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Maaida

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net