Al-Maaida 5:35
المائدةيَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ ٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ وَٱبْتَغُوٓا۟ إِلَيْهِ ٱلْوَسِيلَةَ وَجَـٰهِدُوا۟ فِى سَبِيلِهِۦ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ
Enyi mlioamini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na tafuteni njia ya kumfikia. Na pambaneni kwa juhudi katika njia yake ili mfaulu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na tafuteni njia ya kumfikilia. Na wanieni kwa juhudi kwa ajili yake ili mpate kuokoka. [35]
[35] Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu kwa kujitenga na anayo yakataza, na kut'ii amri zake. Na takeni kuyafanya yatakayo kukurubisheni kupata thawabu zake, nayo ni kutenda mambo ya ut'iifu na mambo ya kheri. Na wanieni kwa jihadi katika Njia yake kwa kuitukuza Dini yake na kuwapiga vita maadui zake. Huenda kwa hivyo mkafuzu mkapata karama zake na thawabu zake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Enyi mliomuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake na mkafuata Sheria Yake kivitendo, muogopeni Allah Mtukufu na mjisogeze karibu Kwake kwa kumtii na kufanya yanayomridhisha, na mpigane jihadi katika njia Yake ili mpate kufaulu kwa kuingia mabustani ya Pepo Yake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net