Al-Maaida 5:34
المائدةإِلَّا ٱلَّذِينَ تَابُوا۟ مِن قَبْلِ أَن تَقْدِرُوا۟ عَلَيْهِمْ ۖ فَٱعْلَمُوٓا۟ أَنَّ ٱللَّهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ
Isipokuwa wale waliotubia kabla hamjawatia nguvuni. Basi jueni kwamba hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kufuta dhambi, Mwenye kurehemu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Isipo kuwa wale walio tubu kabla hamjawatia nguvuni. Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye maghfira na Mwenye kurehemu. [34]
[34] Ila wale walio tubu, miongoni mwa hawa wanao piga vita nidhamu na wakavamia watu majiani, kabla hamjawatia mkononi mkawakamata. Basi adhabu ya Mwenyezi Mungu itaondoka, itabaki juu yao haki za waja wa Mwenyezi Mungu wazirejeshe. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghfira na rehema. Katika hukumu hii inabainishwa kuwa Sharia inaangalia ukhalifu unao athiri jamii, na kwa hivyo adhabu yake ni kali kwa kuwafikiana na kitisho chake kwa wapendao amani. Mazingatio hapa si kwa mujibu wa kile kitendo cha ukhalifu, bali kwa mujibu wa kiasi ya kitisho na fazaa inayo letwa na hicho kitendo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Lakini atakayekuja kati ya wale wanaopiga vita kabla hamjawatia mkononi na akaja akiwa mtiifu mwenye majuto, atafutiwa yale yaliyokuwa ni haki ya Allah Mtukufu. Na jueni, enyi Waumini, kwamba Allah Mtukufu ni Mwingi wa msamaha kwa waja Wake, ni Mwenye kuwarehemu .
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net