Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 5 · Aya ya 33

Al-Maaida 5:33

المائدة

إِنَّمَا جَزَٰٓؤُا۟ ٱلَّذِينَ يُحَارِبُونَ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ وَيَسْعَوْنَ فِى ٱلْأَرْضِ فَسَادًا أَن يُقَتَّلُوٓا۟ أَوْ يُصَلَّبُوٓا۟ أَوْ تُقَطَّعَ أَيْدِيهِمْ وَأَرْجُلُهُم مِّنْ خِلَـٰفٍ أَوْ يُنفَوْا۟ مِنَ ٱلْأَرْضِ ۚ ذَٰلِكَ لَهُمْ خِزْىٌ فِى ٱلدُّنْيَا ۖ وَلَهُمْ فِى ٱلْـَٔاخِرَةِ عَذَابٌ عَظِيمٌ

Maana

Basi malipo ya wale wanaompiga vita Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na wakawania kufanya uharibifu katika nchi, ni kuuawa, au kusulibiwa, au kukatwa mikono yao na miguu yao kwa mabadilisho, au kutolewa nchini. Hii ndiyo hizaya yao katika dunia; na katika Akhera wana adhabu kubwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Basi malipo ya wale wanao mpiga vita Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wakawania kufanya uchafuzi katika nchi, ni kuuwawa, au kusalibiwa, au kukatwa mikono yao na miguu yao kwa mabadilisho, au kutolewa nchi. Hii ndiyo hizaya yao katika dunia; na katika Akhera watapata adhabu kubwa. [33]

[33] Hakika adhabu ya wale wanao mpiga vita Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwa kuacha hukumu za Sharia, na wakafanya uharibifu katika nchi kwa uharamia na kunyan'ganya mali, ni kuuliwa pindi wakiuwa, na kutundikwa msalabani, pindi wakiuwa na wakapokonya mali ya watu, na kukatwa mikono yao na miguu kwa mabadilisho (yaani mkono wa kulia na mguu wa kushoto, au kinyume cha hayo), pindi ikiwa watavamia watu njiani na kuwapokonya mali bila ya kuwauwa. Na ikiwa watawatisha watu tu, basi adabu yao ni kuhamishwa nchi au wafungwe. Adhabu hizo ni hizaya ya hapa duniani tu, na Akhera watapata adhabu kuu, nayo ni adhabu ya Motoni.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika malipo ya wale wanaompiga vita Allah Mtukufu na wanaojitokeza wazi kumfanyia uadui na kuzifanyia uadui hukumu zake na hukumu za Mtume Wake na kufanya uharibifu katika ardhi kwa kuwaua watu na kupora mali, ni wauawe au wasulubiwe pamoja na kuuawa (Kusululubiwa ni kufungwa mhalifu juu ya bao) au ukatwe mkono wa kulia wa mpiga vita na mguu wake wa kushoto. Iwapo hatatubu{kwa kuendelea na uharamia wake}, ukatwe mkono wake wa kushoto na mguu wa kulia, au wahamishwe wapelekwe mji usiokuwa wao, wafungwe kwenye jela ya mji huo mpaka ionekane toba yao. Na haya ndiyo malipo Aliyoyaandika Allah Mtukufu kwa wenye kupiga vita; nayo ni unyonge wa duniani. Na huko Akhera itawapata adhabu kali iwapo hawatatubia.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Maaida

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net