Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 5 · Aya ya 36

Al-Maaida 5:36

المائدة

إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ لَوْ أَنَّ لَهُم مَّا فِى ٱلْأَرْضِ جَمِيعًا وَمِثْلَهُۥ مَعَهُۥ لِيَفْتَدُوا۟ بِهِۦ مِنْ عَذَابِ يَوْمِ ٱلْقِيَـٰمَةِ مَا تُقُبِّلَ مِنْهُمْ ۖ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ

Maana

Hakika wale waliokufuru lau yangelikuwa yao ni yote yaliyo katika dunia, na mfano wake pamoja na hayo, ili watoe kwayo fidia ya kuepukana na adhabu ya Siku ya Kiyama, yasingelikubaliwa kutoka kwao; na wana adhabu chungu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hakika walio kufuru lau wange kuwa na yote yaliyomo duniani, na mengine kama hayo, ili watoe fidia ya kuepukana na adhabu ya Siku ya Kiyama, yasingeli pokelewa kwao; na watapata adhabu chungu. [36]

[36] Hakika walio kufuru hata lau kuwa wana kila namna ya mali yote yaliyomo duniani na mambo mengine yanayo onekana yenye maana katika uhai, na wakawa nayo mfano wa yaliyomo duniani juu ya hayo yaliomo humo, na wakataka yawe ni fidiya wajiokoe na adhabu ya Mwenyezi Mungu Siku ya Kiyama kwa ukafiri wao, basi fidiya hiyo yote haitofaa kitu. Wala Mwenyezi Mungu hawakubalii hayo. Hapana njia yo yote ya wao kuepukana na malipo ya ukafiri wao; nao watapata adhabu kali.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika wale walioukanusha upweke wa Allah Mtukufu na sheria Yake, lau wangekuwa wao wamemiliki vyote vilivyoko ardhini na wakavimiliki vyingine mfano wake, na wakataka kuzikomboa nafsi zao, Siku ya Kiyama, na adhabu ya Allah Mtukufu kwa hivyo walivyovimiliki, Allah Mtukufu Hangalikubali hilo. Na itawapata wao adhabu yenye kuumiza.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Maaida

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net