Al-Maaida 5:37
المائدةيُرِيدُونَ أَن يَخْرُجُوا۟ مِنَ ٱلنَّارِ وَمَا هُم بِخَـٰرِجِينَ مِنْهَا ۖ وَلَهُمْ عَذَابٌ مُّقِيمٌ
Wanataka kwamba watoke Motoni, lakini hawawezi kutoka humo, na wana adhabu inayodumu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Watataka watoke Motoni, lakini hawatatoka humo, na watakuwa na adhabu inayo dumu. [37]
[37] Hawa makafiri wanatamani kutoka Motoni, na wala hawatatoka humo. Watapata adhabu ya daima dawamu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Makafiri hawa watataka watoke Motoni kwa ajili ya visanga vyake wanavyovipata, lakini hawatakuwa na njia yoyote ya kufanya hivyo. Na watakuwa na adhabu ya kudumu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net