Al-Maaida 5:38
المائدةوَٱلسَّارِقُ وَٱلسَّارِقَةُ فَٱقْطَعُوٓا۟ أَيْدِيَهُمَا جَزَآءًۢ بِمَا كَسَبَا نَكَـٰلًا مِّنَ ٱللَّهِ ۗ وَٱللَّهُ عَزِيزٌ حَكِيمٌ
Na mwizi mwanamume na mwizi mwanamke, ikateni mikono yao, yakiwa ni malipo ya waliyoyachuma, ndiyo adhabu ya mfano itokayo kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na mwizi mwanamume na mwizi mwanamke, ikateni mikono yao, hayo ni malipo ya waliyo yachuma, ndiyo adhabu ya mfano itokayo kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu na Mwenye hikima. [38]
[38] Na mwanamume aliye iba, na mwanamke aliye iba, ikateni mikono yao kuwa ni malipo ya madhambi waliyo yatenda, na njia ya kuwaonya wenginewe wasitende jambo hilo. Hiyo ni hukumu ya Mwenyezi Mungu, na amri ya Mwenyezi Mungu ndiyo yenye kushinda, naye ndiye Mwenye hikima katika kutunga Sharia. Kila ukhalifu ameuwekea malipo yake, yenye kumzuia mtu asitende tena na wengine watahadhari wasifanye kama hayo. (Ajabu iliopo ni kuwepo wajinga wakashtushwa na amri hii ya Mwenyezi Mungu aliye tuumba, na wasiseme lolote kuwa katika China wakati wa vita na Taiwan ilikuwapo sharia ya kuwa mwizi auwawe, na katika baadhi ya wilaya za Amerika mpaka hii leo ipo sharia ya kuwa mwizi wa farasi auwawe, na katika Kenya adabu ya wizi wa kutumia nguvu ni kunyongwa, na katika sharia za Kiingereza na nchi zote za magharibi mtu ana haki ya kuuwa kwa ajili ya kulinda mali na roho. Ikiwa ni haki ya mtu kumuuwa atakaye kuja kwiba, jee ni kuu hilo kwa serikali kumkata mkono aliye kwisha iba?) Kwa kuwepo sharia kama hii ndiyo ikawa wizi umetoweka katika nchi kama Saudi Arabia, na ukawa vururu kwengineko.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na mwizi wa kiume na mwizi wa kike, wakateni, enyi watawala, mikono yao kuambatana na Sheria. Hayo yakiwa ni malipo yao kwa kuchukua kwao mali ya watu pasi na haki, na ni mateso ambayo kwayo Allah Mtukufu Anawazuia wengineo kufanya mfano wa kitendo chao. Na Allah Mtukufu ni Mshindi katika mamlaka Yake, ni Mwenye hekima katika amri Zake na makatazo Yake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net