Al-Maaida 5:39
المائدةفَمَن تَابَ مِنۢ بَعْدِ ظُلْمِهِۦ وَأَصْلَحَ فَإِنَّ ٱللَّهَ يَتُوبُ عَلَيْهِ ۗ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ
Lakini mwenye kutubia baada ya dhuluma yake, na akatengenea, basi Mwenyezi Mungu ataipokea toba yake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kufuta dhambi, Mwenye kurehemu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Lakini mwenye kutubia baada ya dhulma yake, na akatengenea, basi Mwenyezi Mungu atapokea toba yake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye maghfira na Mwenye kurehemu. [39]
[39] Lakini mwenye kutubu baada ya kutenda kosa lake hilo, na akatengeneza vitendo vyake, na akanyoosha mwendo wake, basi Mwenyezi Mungu hakika humkubalia toba yake. Hakika Mwenyezi Mungu ni mwingi mno wa kusamehe na kurehemu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Basi yule atakayetubia baada ya wizi wake na akawa mwema katika vitendo vyake vyote, kwa hakika Allah Mtukufu Ataikubali toba yake. Hakika Allah Mtukufu ni Mwenye kuwasamehe waja Wake, ni Mwenye huruma kwao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net