Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 5 · Aya ya 40

Al-Maaida 5:40

المائدة

أَلَمْ تَعْلَمْ أَنَّ ٱللَّهَ لَهُۥ مُلْكُ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ يُعَذِّبُ مَن يَشَآءُ وَيَغْفِرُ لِمَن يَشَآءُ ۗ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ قَدِيرٌ

Maana

Je, hukujua ya kwamba Mwenyezi Mungu anao ufalme wa mbingu na ardhi? Humuadhibu amtakaye, na humsamehe amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hujui ya kwamba Mwenyezi Mungu anao ufalme wa mbingu na ardhi? Humuadhibu amtakaye, na humsamehe amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu. [40]

[40] Jua, ewe mwenye fahamu, kwa ujuzi wa yakini, ya kwamba ni Mwenyezi Mungu peke yake ndiye Mwenye kumiliki kila kitu kiliomo katika mbingu na ardhi. Yeye humpa adhabu yake amtakaye, kwa hikima yake na uwezo wake. Na humsamehe amtakaye, kwa hikima yake na rehema yake. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kwani hujui, ewe Mtume, kwamba Allah Mtukufu ni Muumba wa ulimwengu, ni Mwenye kuuendesha na Mwenye kuumiliki na kwamba Yeye, Aliyetukuka, Ndiye Mfanya wa Alitakalo, Anamuadhibu Amtakaye na Anamsamehe Amtakaye; na Yeye juu ya kila kitu ni Muweza.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Maaida

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net