Al-Maaida 5:41
المائدةيَـٰٓأَيُّهَا ٱلرَّسُولُ لَا يَحْزُنكَ ٱلَّذِينَ يُسَـٰرِعُونَ فِى ٱلْكُفْرِ مِنَ ٱلَّذِينَ قَالُوٓا۟ ءَامَنَّا بِأَفْوَٰهِهِمْ وَلَمْ تُؤْمِن قُلُوبُهُمْ ۛ وَمِنَ ٱلَّذِينَ هَادُوا۟ ۛ سَمَّـٰعُونَ لِلْكَذِبِ سَمَّـٰعُونَ لِقَوْمٍ ءَاخَرِينَ لَمْ يَأْتُوكَ ۖ يُحَرِّفُونَ ٱلْكَلِمَ مِنۢ بَعْدِ مَوَاضِعِهِۦ ۖ يَقُولُونَ إِنْ أُوتِيتُمْ هَـٰذَا فَخُذُوهُ وَإِن لَّمْ تُؤْتَوْهُ فَٱحْذَرُوا۟ ۚ وَمَن يُرِدِ ٱللَّهُ فِتْنَتَهُۥ فَلَن تَمْلِكَ لَهُۥ مِنَ ٱللَّهِ شَيْـًٔا ۚ أُو۟لَـٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ لَمْ يُرِدِ ٱللَّهُ أَن يُطَهِّرَ قُلُوبَهُمْ ۚ لَهُمْ فِى ٱلدُّنْيَا خِزْىٌ ۖ وَلَهُمْ فِى ٱلْـَٔاخِرَةِ عَذَابٌ عَظِيمٌ
Ewe Mtume! Wasikuhuzunishe wale wanaokimbilia kukufuru, miongoni mwa wale waliosema kwa vinywa vyao, "Tumeamini", na hali nyoyo zao hazikuamini, na miongoni mwa Mayahudi, wanaosikiliza sana uongo, wanaowasikiliza sana kaumu wengine ambao hawajakujia. Wao huyabadilisha maneno baada ya kuwekwa pahali pake. Wanasema, "Mkipewa haya, basi yachukueni, na msipopewa haya, tahadharini." Na yule ambaye Mwenyezi Mungu anataka kumfitini, basi huwezi kuwa na uwezo kwa ajili yake mbele ya Mwenyezi Mungu. Hao ndio ambao Mwenyezi Mungu hataki kuzisafisha nyoyo zao. Wana hizaya katika dunia, na Akhera wana adhabu kubwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Ewe Mtume! Wasikuhuzunishe wa fanyao haraka kukufuru, miongoni mwa wanao sema kwa vinywa vyao: Tumeamini, na hali nyoyo zao hazikuamini, na miongoni mwa Mayahudi, wanao sikiliza kwa ajili ya uwongo, wanao sikiliza kwa ajili ya watu wengine wasio kufikia. Wao huyabadilisha maneno kutoka pahala pake. Wanasema: Mkipewa haya basi yashikeni, na msipo pewa haya tahadharini. Na mtu ambaye Mwenyezi Mungu anataka kumfitini huwezi kuwa na madaraka naye mbele ya Mwenyezi Mungu. Hao ndio ambao Mwenyezi Mungu hataki kuzitakasa nyoyo zao. Watakuwa na hizaya duniani, na Akhera watakuwa na adhabu kubwa. [41]
[41] Ewe Mtume! Visikuhuzunishe vitendo vya makafiri wanao wania ukafiri wa kila aina, hawa wadanganyifu wenye khadaa wasemao kwa ndimi zao: Tumeamini, ilhali nyoyo zao hazifuati haki. Na miongoni mwa Mayahudi wapo wanao kithiri kusikiliza uzushi wa makohani wao na wanayakubali, na wanakisikiliza na kukikubali kikundi maalumu miongoni mwao, na hawaji barazani kwako kwa sababu ya kiburi na chuki! Na hawa huyageuza maneno ya Taurati kutokana pahala pake, baada ya Mwenyezi Mungu kwisha yasimamisha na kuyahukumia! Nao huwaambia wafwasi wao: Mkipewa maneno haya yaliyo potoshwa na kubadilishwa yakubalini na muyafuate. Na kama mkipewa mengine tahadharini nayo msiyakubali. Basi, ewe Mtume! Usihuzunike Mwenyezi Mungu akimhukumia mtu kupotea kwa kumziba moyo wake, wewe hutoweza kumwongoa, au kumnafiisha kwa chochote asicho mtakia Mwenyezi Mungu. Na hao ndio walio pita mipaka katika upotovu na inda. Mwenyezi Mungu Mwenyewe hakutaka kuzisafisha nyoyo zao na uchafu wa chuki, na inadi, na ukafiri. Duniani watapata madhila, kwa kufedheheka na kushindwa, na Akhera watapata adhabu kuu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Ewe Mtume! Wasikuhuzunishe wale ambao wanakimbilia kuukanusha unabii wako miongoni mwa wanafiki ambao wameonyesha Uislamu na huku nyoyo zao ni tupu, kwani mimi ni Mwenye kukuokoa na wao. Na lisikuhuzunishe lile la kukimbilia kwa Mayahudi kuukanusha unabii wako, kwani wao ni watu wanaosikiliza urongo, wanayakubali yanayozuliwa na wanavyuoni wao na wanawasikiliza watu wengine wasiohudhuria kwenye baraza yako; na wengine hawa wanayageuza maneno ya Allah Mtukufu baada ya kuyaelewa na wanasema, «Yakiwajia kutoka kwa Muhammad yanayolingana na yale tuliyoyageuza na tukayapotosha katika hukumu za Taurati, basi yatumieni. Na yakiwajia kutoka kwake yanayokwenda kinyume na hayo, basi jihadharini kuyakubali na kuyatumia.» Na ambaye Allah Mtukufu Anataka apotee, basi hutaweza, ewe Mtume, kulizuia hilo lisiwe kwake na wala huwezi kumuongoza.. Na hakika hawa wanafiki na Mayahudi, Allah Mtukufu Hakutaka kuzitakasa nyoyo zao na uchafu wa ukafiri, wana udhalilifu na fedheha hapa duniani, na watapata, huko Akhera, adhabu kubwa.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net