Al-Maaida 5:42
المائدةسَمَّـٰعُونَ لِلْكَذِبِ أَكَّـٰلُونَ لِلسُّحْتِ ۚ فَإِن جَآءُوكَ فَٱحْكُم بَيْنَهُمْ أَوْ أَعْرِضْ عَنْهُمْ ۖ وَإِن تُعْرِضْ عَنْهُمْ فَلَن يَضُرُّوكَ شَيْـًٔا ۖ وَإِنْ حَكَمْتَ فَٱحْكُم بَيْنَهُم بِٱلْقِسْطِ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ يُحِبُّ ٱلْمُقْسِطِينَ
Hao ni wasikilizaji sana wa uongo, na ni walaji mno vya haramu! Basi wakikujia, wahukumu baina yao au wapuuze. Na ukiwapuuza, basi wao hawatakudhuru kitu. Na ukiwahukumu, basi hukumu baina yao kwa uadilifu. Hakika Mwenyezi Mungu anawapenda waadilifu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hao ni wasikilizaji kwa ajili ya kusema uwongo, na ni walaji mno vya haramu! Basi wakikujia, wahukumu baina yao au jipuuze nao. Na ukijipuuza nao, basi wao hawatakudhuru kitu. Na ukiwahukumu, basi hukumu baina yao kwa uadilifu. Hakika Mwenyezi Mungu anawapenda waadilifu. [42]
[42] Hao hukithiri kusikiliza ili wapate kuzua, na hukithiri kula mali ya haramu ambayo hayana baraka yoyote, kama vile rushwa na riba na mengineyo. Basi wakikujia kukutaka uwahukumu, wewe wahukumu pindi ukiona hayo yana maslaha, au jipuuze nao. Na ukijipuuza nao hawatokudhuru kwa lolote, kwa kuwa Mwenyezi Mungu ndiye wa kukulinda na watu. Na ukihukumu baina yao basi hukumu kwa uadilifu alio kuamrisha Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda waadilifu, naye huwahifadhi na huwalipa thawabu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Mayahudi hawa wanakusanya kati ya usikilizaji urongo na ulaji haramu. Basi watakapokujia wakishtakiana kwako, basi hukumu kati yao au waache. Na usipohukumu kati yao, hawataweza kukudhuru kwa chochote. Na iwapo utahukumu, basi hukumu kati yao kwa uadilifu. Hakika Allah Mtukufu Anawapenda waadilifu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net