Al-Maaida 5:43
المائدةوَكَيْفَ يُحَكِّمُونَكَ وَعِندَهُمُ ٱلتَّوْرَىٰةُ فِيهَا حُكْمُ ٱللَّهِ ثُمَّ يَتَوَلَّوْنَ مِنۢ بَعْدِ ذَٰلِكَ ۚ وَمَآ أُو۟لَـٰٓئِكَ بِٱلْمُؤْمِنِينَ
Na vipi wanakufanya kuwa hakimu wao ilhali wanayo Taurati yenye hukumu za Mwenyezi Mungu ndani yake? Kisha baada ya hayo wanageuka. Na hao si Waumini.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na huwaje wakufanye wewe hakimu nao wanayo Taurati yenye hukumu za Mwenyezi Mungu? Kisha baada ya hayo wanageuka. Na hao si wenye kuamini. [43]
[43] Ama ajabu ya watu hawa Mayahudi! Vipi wanataka hukumu yako na hali wao wanayo hukumu ya Mwenyezi Mungu imeandikwa katika Taurati? Na kinacho staajabisha ni kuwa wao huikataa hukumu yako inapo kuwa haikubaliani na mapendeleo yao, ijapo kuwa imewafikiana na ilivyo katika kitabu chao! Watu hawa sio miongoni mwa Waumini wanaoit'ii Haki.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kitendo cha Mayahudi hawa ni cha kushangaza. Wao wanashitakiana kwako, ewe Mtume, na wao hawakuamini wewe wala Kitabu chako, pamoja na kuwa ile Taurati wanayoiamini wanayo, na humo muna hukumu ya Allah Mtukufu; kisha wanaondoka baada ya kutoa hukumu yako, iwapo haikuwaridhisha, wakakusanya kati ya kuzikataa sheria zao na kuipa mgongo hukumu yako. Na hawakuwa hao, wanaosifika na sifa hizo, ni wenye kumuamini Allah Mtukufu, kukuamini wewe na kuikubali hukumu uliyoitoa.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net