Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 5 · Aya ya 16

Al-Maaida 5:16

المائدة

يَهْدِى بِهِ ٱللَّهُ مَنِ ٱتَّبَعَ رِضْوَٰنَهُۥ سُبُلَ ٱلسَّلَـٰمِ وَيُخْرِجُهُم مِّنَ ٱلظُّلُمَـٰتِ إِلَى ٱلنُّورِ بِإِذْنِهِۦ وَيَهْدِيهِمْ إِلَىٰ صِرَٰطٍ مُّسْتَقِيمٍ

Maana

Mwenyezi Mungu huwaongoa kwacho wenye kufuata radhi yake katika njia za salama, na huwatoa katika giza mbalimbali na kuwapeleka kwenye nuru kwa idhini yake, na huwaongoa kwenye Njia iliyonyooka.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Mwenyezi Mungu huwaongoa wenye kufuata radhi yake katika njia za salama, na huwatoa katika giza kuwapeleka kwenye nuru kwa amri yake, na huwaongoa kwenye njia iliyo nyooka. [16]

[16] Mwenyezi Mungu kwa Kitabu hichi anawaongoa kwenye njia ya uwokofu wanao elekea kutaka radhi zake, na anawatoa kwenye giza la ukafiri kuendea mwangaza wa Imani kwa tawfiki yake, na anawaongoza kwenye njia ya Haki.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kwa kitabu hiki chenye ufafanuzi, Allah Mtukufu Anawaongoza wenye kufuata yenye kumridhi Allah Mtukufu, Aliyetukuka, njia za amani na usalama, Anawatoa kutoka kwenye giza la ukafiri kuwapeleka kwenye mwangaza wa Imani na Anawaafikia wao kufuata dini Yake iliyonyooka.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Maaida

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net