Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 5 · Aya ya 15

Al-Maaida 5:15

المائدة

يَـٰٓأَهْلَ ٱلْكِتَـٰبِ قَدْ جَآءَكُمْ رَسُولُنَا يُبَيِّنُ لَكُمْ كَثِيرًا مِّمَّا كُنتُمْ تُخْفُونَ مِنَ ٱلْكِتَـٰبِ وَيَعْفُوا۟ عَن كَثِيرٍ ۚ قَدْ جَآءَكُم مِّنَ ٱللَّهِ نُورٌ وَكِتَـٰبٌ مُّبِينٌ

Maana

Enyi Watu wa Kitabu! Hakika amekwishawajia Mtume wetu anayewabainishia mengi katika yale mliyokuwa mkiyaficha katika Kitabu, na anayaacha mengi. Bila shaka imekwishawajia kutoka kwa Mwenyezi Mungu nuru na Kitabu kilicho wazi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Enyi Watu wa Kitabu! Amekwisha kujieni Mtume wetu anaye kufichulieni mengi mliyo kuwa mkiyaficha katika Kitabu, na anaye samehe mengi. Bila shaka imekujieni kutoka kwa Mwenyezi Mungu nuru na Kitabu kinacho bainisha. [15]

[15] Enyi Watu wa Kitabu! Amekujilieni Mtume wetu, Muhammad, akiita watu wafuate Haki. Anakufichulieni mengi mliyo kuwa mkiyaficha katika Taurati na Injili. Na anayaacha mengi katika mliyo yaficha ambayo hayana haja kuyadhihirisha. Amekuleteeni kutoka kwa Mwenyezi Mungu Sharia kaamili, ambayo Sharia hiyo peke yake ni nuru, na inabainishwa na Kitabu kilicho wazi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Enyi watu mliopewa Kitabu, miongoni mwa Mayahudi na Wanaswara! Amewajia nyinyi mjumbe wetu Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie, kuwafafanulia mengi ambayo mlikuwa mkiyaficha kwa watu katika yale yaliyomo ndani ya Taurati na Injili, na anaacha kubainisha yasio endana na hekma. Hakika umewajia kutoka kwa Allah Mtukufu mwangaza na Kitabu chenye ufafanuzi, nacho ni Qur’ani tukufu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Maaida

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net