Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 5 · Aya ya 14

Al-Maaida 5:14

المائدة

وَمِنَ ٱلَّذِينَ قَالُوٓا۟ إِنَّا نَصَـٰرَىٰٓ أَخَذْنَا مِيثَـٰقَهُمْ فَنَسُوا۟ حَظًّا مِّمَّا ذُكِّرُوا۟ بِهِۦ فَأَغْرَيْنَا بَيْنَهُمُ ٱلْعَدَاوَةَ وَٱلْبَغْضَآءَ إِلَىٰ يَوْمِ ٱلْقِيَـٰمَةِ ۚ وَسَوْفَ يُنَبِّئُهُمُ ٱللَّهُ بِمَا كَانُوا۟ يَصْنَعُونَ

Maana

Na kutoka kwa wale waliosema: 'Sisi ni Manasara', tulichukua agano lao, lakini wakasahau sehemu katika yale waliyokumbushwa kwayo. Kwa hivyo tukaweka kati yao uadui na chuki mpaka Siku ya Qiyama. Na hapo Mwenyezi Mungu atawaambia yale waliyokuwa wakiyafanya.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na kutoka kwa wale walio sema: Sisi ni Manasara, tulichukua ahadi yao, lakini wakasahau sehemu ya waliyo kumbushwa. Kwa hivyo tukaweka kati yao uadui na chuki mpaka Siku ya Kiyama. Na hapo Mwenyezi Mungu atawaambia waliyo kuwa wakiyafanya. [14]

[14] Hali kadhaalika Mwenyezi Mungu alichukua ahadi kwa Wakristo, ambao wamesema: Sisi ni Manasara, kwa kuwa wataiamini Injili, na watamuamini Mwenyezi Mungu Mmoja. Nao wakaacha mengi walio amrishwa katika Injili. Mwenyezi Mungu akawaadhibu kwa hayo, kwa kutia uadui na khasama baina ya wao kwa wao, wakawa makundi mbali mbali yenye uadui mpaka Siku ya Kiyama. Na hapo Mwenyezi Mungu atawaambia waliyo kuwa wakiyafanya, na atawalipa kwayo.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na tulichukua ahadi ya mkazo kwa wale waliodai kuwa wao ni wafuasi wa Al-Masîḥ ‘Ǐsâ mwana wa Maryam, na hali wao sio hivyo, kama ile tulioichukua kwa Wana wa Isrãîl, kwamba watamfuata Mtume wao, watamnusuru na watamsaidia, lakini walibadilisha Dini yao na wakaacha kutumia sehemu ya yale waliyokumbushwa nayo, kama walivyofanya Mayahudi. Kwa hivyo tulitia uadui na chuki kati yao mpaka Siku ya Kiyama. Na Allah Mtukufu Atawapa habari, Siku ya Hesabu, ya yale ambayo wao walikuwa wakiyafanya, na Atawatesa kwa matendo yao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Maaida

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net