Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 5 · Aya ya 17

Al-Maaida 5:17

المائدة

لَّقَدْ كَفَرَ ٱلَّذِينَ قَالُوٓا۟ إِنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلْمَسِيحُ ٱبْنُ مَرْيَمَ ۚ قُلْ فَمَن يَمْلِكُ مِنَ ٱللَّهِ شَيْـًٔا إِنْ أَرَادَ أَن يُهْلِكَ ٱلْمَسِيحَ ٱبْنَ مَرْيَمَ وَأُمَّهُۥ وَمَن فِى ٱلْأَرْضِ جَمِيعًا ۗ وَلِلَّهِ مُلْكُ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا ۚ يَخْلُقُ مَا يَشَآءُ ۚ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ قَدِيرٌ

Maana

Hakika wamekufuru wale waliosema: 'Hakika Mwenyezi Mungu ni Masihi mwana wa Maryam.' Sema: Basi ni nani mwenye kumiliki chochote mbele ya Mwenyezi Mungu ikiwa Yeye angetaka kumwangamiza Masihi mwana wa Maryamu, na mama yake, na wote walio katika ardhi? Na ni wa Mwenyezi Mungu tu ufalme wa mbingu na ardhi na vilivyo kati yake. Huumba apendavyo. Na Mwenyezi Mungu anao uweza juu ya kila kitu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hakika wamekufuru walio sema: Mwenyezi Mungu ni Masihi mwana wa Maryamu. Sema: Ni nani mwenye kumiliki cho chote mbele ya Mwenyezi Mungu ikiwa Yeye angetaka kumuangamiza Masihi mwana wa Maryamu, na mama yake, na wote waliomo katika ardhi? Na mamlaka ya mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake ni vya Mwenyezi Mungu. Huumba apendavyo. Na Mwenyezi Mungu anao uweza juu ya kila kitu. [17]

[17] Hakika wamekufuru wale wanao dai ati Mwenyezi Mungu ndiye Masihi mwana wa Maryamu!! Ewe Mtume! Waambie hao wanao thubutu kuchezea cheo cha Ungu: Hapana ye yote anaye weza kuzuia matakwa ya Mwenyezi Mungu akitaka kumteketeza Isa na mama yake, na kuwahiliki wote waliomo katika ardhi. Kwani ufalme wa mbingu na ardhi na vilivyo baina yao ni wa Mwenyezi Mungu peke yake. Yeye huumba mfano autakao. Na Mwenyezi Mungu ana uweza mkubwa kabisa. Hashindwi na kitu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kwa hakika wamekufuru Wanaswara wanaosema kwamba Allah Mtukufu ni Al-Masîh mwana wa Maryam. Sema, ewe Mtume, kuwaambia Wanaswara hawa wajinga, Lau Al- Masîḥ angalikuwa Mungu, kama wanavyodai, angaliweza kuuzuia uamuzi wa Allah Mtukufu ukimjia wa kumwangamiza yeye na mama yake na watu wote wa ardhini. Na mama yake ‘Ǐsâ alikufa, hakuweza kumkinga na kifo. Vilevile hawezi kujitetea nafsi yake. Kwani wote wawili ni waja miongoni mwa waja wa Allah Mtukufu, hawawezi kujiepusha na maangamivu. Hii ni dalili kuwa yeye ni mwanadamu kama wanadamu wengine. Na vitu vyote vilivyoko mbinguni na ardhini ni milki ya Allah Mtukufu, Anaumba na kupatisha anachotaka na yeye ni muweza wa kila kitu. Hakika ya tawḥîd (kumpwekesha Allah Mtukufu) inawajibisha kupwekeka Allah Mtukufu, Aliyetukuka, kwa sifa za uola na uungu; hakuna yoyote anayeshirikiana naye, katika viumbe Wake, kwa hilo. Na mara nyingi sana watu huingia kwenye ushirikina na upotevu kwa kuwatukuza Mitume na watu wema kupita kiasi, kama walivyopita kiasi Wanaswara katika kumtukuza Al-Masîḥ. Ulimwengu wote ni wa Allah Mtukufu, na viumbe viko kwenye mikono yake Peke Yake. Na miujiza na alama kubwa zinazodhihiri, marejeo yake ni Allah Mtukufu.Anaumba, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, na Anafanya Anachotaka.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Maaida

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net