Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 5 · Aya ya 18

Al-Maaida 5:18

المائدة

وَقَالَتِ ٱلْيَهُودُ وَٱلنَّصَـٰرَىٰ نَحْنُ أَبْنَـٰٓؤُا۟ ٱللَّهِ وَأَحِبَّـٰٓؤُهُۥ ۚ قُلْ فَلِمَ يُعَذِّبُكُم بِذُنُوبِكُم ۖ بَلْ أَنتُم بَشَرٌ مِّمَّنْ خَلَقَ ۚ يَغْفِرُ لِمَن يَشَآءُ وَيُعَذِّبُ مَن يَشَآءُ ۚ وَلِلَّهِ مُلْكُ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا ۖ وَإِلَيْهِ ٱلْمَصِيرُ

Maana

Na Mayahudi na Wakristo walisema: Sisi ni wana wa Mwenyezi Mungu na vipenzi vyake. Sema: Basi kwa nini anawaadhibu kwa sababu ya dhambi zenu? Bali nyinyi ni wanadamu tu kama wale wengine aliowaumba. Humfutia dhambi amtakaye na humuadhibu amtakaye. Na ni wa Mwenyezi Mungu tu ufalme wa mbingu na ardhi na vilivyo kati yake. Na marejeo ni kwake Yeye.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na Mayahudi na Wakristo wanasema: Sisi ni wana wa Mwenyezi Mungu na vipenzi vyake. Sema: Basi kwa nini anakuadhibuni kwa ajili ya dhambi zenu? Bali nyinyi ni watu tu kama wale wengine alio waumba. Humsamehe amtakaye na humuadhibu amtakaye. Na ni wa Mwenyezi Mungu tu ufalme wa mbingu na ardhi. Na marejeo ni kwake Yeye. [18]

[18] Na Mayahudi na Wakristo husema: Sisi ndio tulio fadhiliwa, kwani sisi ndio wana wa Mwenyezi Mungu na vipenzi vyake atupendao. Waambie ewe Mtume! Basi kwa nini anakuadhibuni kwa dhambi zenu, na anakutieni katika moto wa Jahannamu? Waongo nyinyi! Nyinyi, kama wanaadamu wengineo, ni viumbe, na mtahisabiwa kwa vitendo vyenu. Na maghfira yamo mikononi mwa Mwenyezi Mungu peke yake, humsamehe amtakaye. Na adhabu yake ni kwa amtakaye kumuadhibu. Kwani ufalme wa mbingu na ardhi na viliomo baina yao ni wa Mwenyezi Mungu tu, na kwake Yeye ndio marejeo ya mwisho.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Mayahudi na Wanaswara walidai kuwa wao ni wana wa Allah Mtukufu na vipenzi vyake. Sema kuwaambia, ewe Mtume, «Basi ni kwa nini Atawaadhibu kwa madhambi yenu.» Lau mngekuwa ni vipenzi Vyake hangaliwaadhibu. Kwani Allah Mtukufu Hampendi isipokuwa Anayemtii. Na waambie wao, «Bali nyinyi ni viumbe kama walivyo binadamu wengine, mkifanya wema mtalipwa mema kwa wema wenu, na mkifanya ubaya mtalipwa shari kwa ubaya wenu.» Allah Mtukufu Atamsamehe Anayemtaka, na Atamuadhibu Anayemtaka. Yeye Ndiye Anayeumiliki ufalme, Anaupeleka Anavyotaka na Kwake ndio marudio. Na hapo Atatoa uamuzi kwa waja Wake na Atamlipa kila mmoja anachostahiki.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Maaida

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net