Al-Maaida 5:19
المائدةيَـٰٓأَهْلَ ٱلْكِتَـٰبِ قَدْ جَآءَكُمْ رَسُولُنَا يُبَيِّنُ لَكُمْ عَلَىٰ فَتْرَةٍ مِّنَ ٱلرُّسُلِ أَن تَقُولُوا۟ مَا جَآءَنَا مِنۢ بَشِيرٍ وَلَا نَذِيرٍ ۖ فَقَدْ جَآءَكُم بَشِيرٌ وَنَذِيرٌ ۗ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ قَدِيرٌ
Enyi Watu wa Kitabu! Bila ya shaka amewajia Mtume wetu akiwabainishia katika wakati usiokuwa na Mitume, ili msije mkasema: 'Hakutujia mbashiri wala mwonyaji.' Basi kwa hakika amekwisha wajia mbashiri na mwonyaji. Na Mwenyezi Mungu ana uweza juu ya kila kitu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Enyi Watu wa Kitabu! Bila ya shaka amekujilieni Mtume wetu akikubainishieni katika wakati usio kuwa na Mitume, msije mkasema: Hakufika kwetu mbashiri wala mwonyaji. Basi amekujieni mbashiri na mwonyaji. Na Mwenyezi Mungu anao uweza wa kila kitu. [19]
[19] Enyi Watu wa Kitabu! Umekujieni ujumbe wa Mtume wetu ambaye anakudhihirishieni Haki, baada ya kusita ujumbe kwa muda wa zama, ili msitafute udhuru wa ukafiri wenu, kwa kudai ati kuwa Mwenyezi Mungu hakukuleteeni mbashiri wa kukupeni khabari njema, wala mwonyaji wa kukuhadharisheni. Sasa, basi, huyo amekujilieni mbashiri na mwonyaji. Na Mwenyezi Mungu ni muweza wa kila jambo - na katika hayo mambo ni kutuma Mitume, na kukuhisabuni kwa mliyo nayo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Enyi Mayahudi na Wanaswara, amewajia mjumbe wetu Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie,, ili kuwafunulia haki na uongofu baada ya kipindi kirefu cha wakati baina ya kumtuma yeye na kumtuma ‘Ǐsâ mwana wa Maryam, ili msije mkasema, «Hakutujia mjumbe, mwenye kutoa bishara wala mwenye kuonya.» Hakika ashawajia kutoka kwa Allah Mtukufu mjumbe anayempa bishara njema mwenye kumuamini na anayemuonya mwenye kumuasi. Na Allah Mtukufu ni Muweza wa kila kitu, wa kumtesa mwenye kuasi na kumpa thawabu mwenye kutii.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net