Al-Maaida 5:20
المائدةوَإِذْ قَالَ مُوسَىٰ لِقَوْمِهِۦ يَـٰقَوْمِ ٱذْكُرُوا۟ نِعْمَةَ ٱللَّهِ عَلَيْكُمْ إِذْ جَعَلَ فِيكُمْ أَنۢبِيَآءَ وَجَعَلَكُم مُّلُوكًا وَءَاتَىٰكُم مَّا لَمْ يُؤْتِ أَحَدًا مِّنَ ٱلْعَـٰلَمِينَ
Na pale Musa alipowaambia watu wake: Enyi watu wangu! Kumbukeni neema za Mwenyezi Mungu juu yenu, alipowateua Manabii kati yenu, na akawafanya watawala, na akawapa yale ambayo hakuwapa wowote katika walimwengu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na pale Musa alipo waambia watu wake: Enyi watu wangu! Kumbukeni neema za Mwenyezi Mungu zilizo juu yenu, alipo wateuwa Manabii kati yenu, na akakufanyeni watawala, na akakupeni ambayo hakuwapa wowote katika walimwengu. [20]
[20] Na taja, ewe Mtume! pale Musa alipo waambia watu wake: Enyi watu wangu! Zikumbukeni neema za Mwenyezi Mungu kwa kushukuru na kut'ii, kwa kuwa amewateua Manabii wengi miongoni mwenu, na akakufanyeni watukufu kama wafalme baada ya kuwa mlikuwa wanyonge chini ya utawala wa Firauni, na akakupeni neema nyingi nyenginezo ambazo hawajapewa wowote wengineo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na kumbuka, ewe Mtume, pindi aliposema Mûsã, amani imshukie, kuwaambia watu wake, «Enyi Wana wa Isrãîl, Kumbukeni neema ya Allah Mtukufu kwenu, pindi Alipochagua Manabii kati yenu, Akawafanya wafalme, mnayatawala mambo yenu baada ya kuwa mumetawaliwa na Fir‘aun na watu wake. Na hakika Aliwatunuku nyinyi aina mbalimbali za neema ambazo Hakumtunuku nazo yoyote miongoni mwa walimwengu wa zama zenu».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net