Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 5 · Aya ya 21

Al-Maaida 5:21

المائدة

يَـٰقَوْمِ ٱدْخُلُوا۟ ٱلْأَرْضَ ٱلْمُقَدَّسَةَ ٱلَّتِى كَتَبَ ٱللَّهُ لَكُمْ وَلَا تَرْتَدُّوا۟ عَلَىٰٓ أَدْبَارِكُمْ فَتَنقَلِبُوا۟ خَـٰسِرِينَ

Maana

Enyi watu wangu! Ingieni katika nchi takatifu ambayo Mwenyezi Mungu amewaandikia. Wala msirudi nyuma, mkawa wenye kuhasirika.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Enyi watu wangu! Ingieni katika nchi takatifu ambayo Mwenyezi Mungu amekuandikieni. Wala msirudi nyuma, msije mkawa wenye kukhasirika. [21]

[21] Enyi watu wangu! T'iini amri ya Mwenyezi Mungu. Ingieni ardhi takatifu aliyo kujaalieni Mwenyezi Mungu muingie, wala msirejee nyuma kuwaogopa hao watu wake majabari, mkaja kukosa nusura ya Mwenyezi Mungu na radhi zake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

«Enyi watu wangu, Ingieni kwenye ardhi takatifu, yaani iliyotakaswa, nayo ni Bait al-Maqdis na sehemu zilizo kando-kando yake, ambayo Allah Mtukufu Ametoa ahadi muingie na mkapigane na makafiri waliyo humo wala msirudi nyuma mkaacha kupigana na hao majabari, kwani mkifanya hivyo mtaikosa heri ya duniani na heri ya Akhera».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Maaida

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net