Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 49 · Aya ya 13

Al-Hujuraat 49:13

الحجرات

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ إِنَّا خَلَقْنَـٰكُم مِّن ذَكَرٍ وَأُنثَىٰ وَجَعَلْنَـٰكُمْ شُعُوبًا وَقَبَآئِلَ لِتَعَارَفُوٓا۟ ۚ إِنَّ أَكْرَمَكُمْ عِندَ ٱللَّهِ أَتْقَىٰكُمْ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلِيمٌ خَبِيرٌ

Maana

Enyi watu! Hakika Sisi tumewaumba kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliye mcha Mungu zaidi katika nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua mno, Mwenye habari.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliye mchamngu zaidi katika nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye khabari. [13]

[13] Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni nyinyi sawa sawa kutokana na asli moja, ya Adamu na Hawa. Na tukakufanyeni mkawa wengi kwa mataifa makubwa na makabila mengi, ili kutimie kujuana na kuawiniana baina yenu, sio kubaguana. Na hakika mwenye cheo cha juu miongoni mwenu kwa Mwenyezi Mungu duniani na Akhera ni yule anaye mcha Yeye zaidi. Hakika Mwenyezi Mungu amevizunguka vitu vyote kwa kuvijua, ni Mwenye khabari za dogo na kubwa la kila jambo.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Enyi watu! Sisi tumewaumba nyinyi kutokana na baba mmoja, (naye ni Ᾱdam), na mama mmoja, (naye ni Ḥawwā’), hivyo basi hakuna kufadhilishana baina yenu kinasaba, na tumewafanya nyinyi kwa kuzaana kuwa mataifa na makabila mbalimbali ili mjuane nyinyi kwa nyinyi, hakika mbora wenu zaidi mbele ya Allah Mtukufu ni yule anayemcha Yeye zaidi. Hakika Allah Mtukufu Anawajua sana wachamungu na Anawatambua.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Hujuraat

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net