Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 49 · Aya ya 14

Al-Hujuraat 49:14

الحجرات

قَالَتِ ٱلْأَعْرَابُ ءَامَنَّا ۖ قُل لَّمْ تُؤْمِنُوا۟ وَلَـٰكِن قُولُوٓا۟ أَسْلَمْنَا وَلَمَّا يَدْخُلِ ٱلْإِيمَـٰنُ فِى قُلُوبِكُمْ ۖ وَإِن تُطِيعُوا۟ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ لَا يَلِتْكُم مِّنْ أَعْمَـٰلِكُمْ شَيْـًٔا ۚ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ

Maana

Mabedui walisema: 'Tumeamini.' Sema: 'Hamjaamini, lakini semeni: 'Tumesilimu.' Kwani Imani haijaingia katika nyoyo zenu. Na mkimtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hatakupunguzieni chochote katika vitendo vyenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe mno, Mwingi wa kurehemu.'

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Mabedui wamesema: Tumeamini. Sema: Hamjaamini, lakini semeni: Tumesilimu. Kwani Imani haijaingia katika nyoyo zenu. Na mkimt'ii Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hatakupunguzieni chochote katika vitendo vyenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu. [14]

[14] Wakaazi wa majangwani wamesema kwa ndimi zao: Tumeamini. Ewe Muhammad! Waambie: Bado hamjaamini; kwa sababu nyoyo zenu bado hazijasadiki hayo mnayo yatamka. Lakini nyinyi semeni: Tumefuata dhaahiri ya Ujumbe wako. Bado Imani haijaingia katika nyoyo zenu. Na mkimt'ii Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwa kweli, hato kunyimeni hata chembe katika malipo ya vitendo vyenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mkubwa wa kuwasamehe waja wake, ni Mwenye rehema kunjufu kwa kila kitu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Waarabu wa majangwani, nao ni Mabedui, walisema, «Tumemuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake Imani iliyokamilika.» Waambie, ewe Nabii, «Msijidai kuwa mna Imani kamilifu, lakini semeni, ‘Tumesilimu.’ na bado Imani haijaingia ndani ya nyoyo zenu. Na mkimtii Allah Mtukufu na Mtume Wake Hatawapunguzia chochote katika thawabu za matendo yenu. Hakika Allah Mtukufu ni Mwingi wa msamaha kwa anayetubia dhambi zake, ni Mwingi wa rehema kwake.» Katika aya hii kuna makemeo kwa mtu anayedhihirisha kuamini na kufuata Sunnah, na hali matendo yake yanashuhudilia kinyume cha hivyo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Hujuraat

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net