Al-Hujuraat 49:15
الحجراتإِنَّمَا ٱلْمُؤْمِنُونَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ بِٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦ ثُمَّ لَمْ يَرْتَابُوا۟ وَجَـٰهَدُوا۟ بِأَمْوَٰلِهِمْ وَأَنفُسِهِمْ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ ۚ أُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلصَّـٰدِقُونَ
Hakika Waumini ni wale waliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake tena wasitie shaka kabisa, na wakapigana Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu kwa mali zao na nafsi zao. Hao ndio wakweli.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hakika Waumini ni wale walio muamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake tena wasitie shaka kabisa, na wakapigana Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu kwa mali yao na nafsi zao. Hao ndio wakweli. [15]
[15] Hakika Waumini wa kweli ni wale ambao wanamuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, kisha hapana shaka yoyote inayo ingia katika nyoyo zao kwa hayo wanayo yaamini; tena wakapigana Jihadi kwa kutoa mali yao na roho zao katika njia ya ut'iifu wa Mwenyezi Mungu. Hao peke yao ndio walio wakweli katika Imani yao.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kwa hakika Waumini ni wale waliomuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake na wakafuata sheria Zake kivitendo, kisha wasiwe na shaka katika Imani yao, na wakatoa mali zao nzuri na roho zao kwa kupigana jihadi katika njia ya Allah Mtukufu, na kumtii Yeye na kutafuta radhi Zake, basi hao ndio wakweli katika Imani Yao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net