Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 49 · Aya ya 16

Al-Hujuraat 49:16

الحجرات

قُلْ أَتُعَلِّمُونَ ٱللَّهَ بِدِينِكُمْ وَٱللَّهُ يَعْلَمُ مَا فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَمَا فِى ٱلْأَرْضِ ۚ وَٱللَّهُ بِكُلِّ شَىْءٍ عَلِيمٌ

Maana

Sema: 'Ati ndio mnamfundisha Mwenyezi Mungu Dini yenu, na hali Mwenyezi Mungu anayajua ya katika mbingu na ardhi, na Mwenyezi Mungu anajua vyema kila kitu?'

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Sema: Ati ndio mnamfundisha Mwenyezi Mungu Dini yenu, na hali Mwenyezi Mungu anayajua ya katika mbingu na ardhi, na Mwenyezi Mungu anajua kila kitu? [16]

[16] Ewe Muhammad! Waambie kwa kuwakanusha ile kauli yao kuwa wameamini: Ndio hivyo ati mnampa khabari Mwenyezi Mungu kuwa nyoyo zenu zimesadiki? Na Mwenyezi Mungu peke yake anajua kila kiliomo katika mbingu na katika ardhi. Na Mwenyezi Mungu amevizunguka vitu vyote kwa ujuzi wake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Waambie, ewe Mtume, hawa Mabedui, «Je mnampasha habari Allah Mtukufu kuhusu dini yenu na yaliyomo kwenye dhamiri zenu, na hali Allah Mtukufu Anavijua vilivyoko mbinguni na ardhini? Na Allah Mtukufu ni Mjuzi wa kila kitu, havifichiki Kwake vilivyomo ndani ya nyoyo zenu vya Imani au vya ukafiri na vya wema au vya ubaya».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Hujuraat

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net