Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 49 · Aya ya 17

Al-Hujuraat 49:17

الحجرات

يَمُنُّونَ عَلَيْكَ أَنْ أَسْلَمُوا۟ ۖ قُل لَّا تَمُنُّوا۟ عَلَىَّ إِسْلَـٰمَكُم ۖ بَلِ ٱللَّهُ يَمُنُّ عَلَيْكُمْ أَنْ هَدَىٰكُمْ لِلْإِيمَـٰنِ إِن كُنتُمْ صَـٰدِقِينَ

Maana

Wanakusimbulia kuwa wamesilimu! Sema: 'Msinisimbulie kwa kusilimu kwenu. Bali Mwenyezi Mungu ndiye aliyewafanyia hisani kwa kukuongoeni kwenye Imani, ikiwa nyinyi ni wakweli.'

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wanakusimbulia kuwa wamesilimu! Sema: Msinisimbulie kwa kusilimu kwenu. Bali Mwenyezi Mungu ndiye aliye kufanyieni hisani kwa kukuongoeni kwenye Imani, ikiwa nyinyi ni wakweli. [17]

[17] Wanaona kuwa kusilimu kwao ni kukuunga mkono wewe, Muhammad, na hivyo inastahiki wewe uwashukuru. Sema: Msinisimbulie kusilimu kwenu; kwani kheri yake mnaipata nyinyi. Bali ni Mwenyezi Mungu peke yake ndiye aliye kufanyieni ihsani kwa kukuongoeni kwenye Imani, ikiwa nyinyi ni wakweli katika hayo madai yenu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hawa Mabedui wanakusimbulia wewe, (ewe Nabii), kusilimu kwao, na kukufuata wewe na kukunusuru. Waambie, «msinisimbulie mimi kuingia kwenu kwenye Uislamu, kwani manufaa yake yanawarudia nyinyi wenyewe. Na Allah Mtukufu Ndiye aliyewapa fadhla nyinyi na taufiki ya kumuamini Yeye na Mtume Wake, iwapo nyinyi ni wakweli katika kuamini kwenu».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Hujuraat

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net