Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 49 · Aya ya 12

Al-Hujuraat 49:12

الحجرات

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ ٱجْتَنِبُوا۟ كَثِيرًا مِّنَ ٱلظَّنِّ إِنَّ بَعْضَ ٱلظَّنِّ إِثْمٌ ۖ وَلَا تَجَسَّسُوا۟ وَلَا يَغْتَب بَّعْضُكُم بَعْضًا ۚ أَيُحِبُّ أَحَدُكُمْ أَن يَأْكُلَ لَحْمَ أَخِيهِ مَيْتًا فَكَرِهْتُمُوهُ ۚ وَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ تَوَّابٌ رَّحِيمٌ

Maana

Enyi mlioamini! Jiepusheni na dhana nyingi, kwani baadhi ya dhana ni dhambi. Wala msipelelezane, wala msisengenyane nyinyi kwa nyinyi. Je, yupo katika nyinyi anayependa kuila nyama ya nduguye aliyekufa? Mnalichukia hilo! Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kupokea toba mno, Mwingi wa kurehemu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Enyi mlio amini! Jiepusheni na dhana nyingi, kwani baadhi ya dhana ni dhambi. Wala msipelelezane, wala msisengenyane nyinyi kwa nyinyi. Je! Yupo katika nyinyi anaye penda kuila nyama ya nduguye aliye kufa? Mnalichukia hilo! Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kupokea toba, Mwenye kurehemu. [12]

[12] Enyi mlio amini, jitengeni mbali na wingi wa kudhania dhana mbovu kwa watu wa kheri. Kwani hakika baadhi ya dhana ni dhambi zinazo stahiki adhabu. Wala msiwe mkitafuta aibu za Waislamu. Wala msisengenyane, yaani kumsema mtu nyuma yake kwa jambo linalo muudhi. Hebu yupo yeyote kati yenu anaye penda kula nyama ya nduguye aliye kufa? Bila ya shaka hayo yanakuchukizeni! Basi ichukieni pia tabia ya kusengenyana na kusemana, kwani haya nayo ni mfano wa hayo. Na zikingeni nafsi zenu na adhabu ya Mwenyezi Mungu kwa kufuata amri zake, na kuyaepuka ayakatazayo. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mkubwa wa kukubali toba ya wenye kutubia, Mwenye rehema kunjufu kwa walimwengu wote.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Enyi mliomuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake na mkafuata Sheria Zake kivitendo, Jiepusheni na dhana mbaya kwa Waumini, kwani dhana nyingine ni dhambi. Wala msipekue aibu za Waislamu, wala msisemane nyinyi kwa nyinyi maneno yenye kuchukiwa na wenye kusemwa na hali wao hawapo. Je, anapenda mmoja wenu kula nyama ya ndugu yake akiwa amekufa? Nyinyi mnalichukia hilo, basi lichukieni lile la kumsengenya. Na muogopeni Allah Mtukufu katika yale Aliyowaamrisha na kuwakataza. Hakika Allah Mtukufu ni Mwingi wa kukubali toba za waja Wake Waumini, ni Mwingi wa rehema kwao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Hujuraat

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net