Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 43 · Aya ya 87

Az-Zukhruf 43:87

الزخرف

وَلَئِن سَأَلْتَهُم مَّنْ خَلَقَهُمْ لَيَقُولُنَّ ٱللَّهُ ۖ فَأَنَّىٰ يُؤْفَكُونَ

Maana

Na ukiwauliza ni nani aliyewaumba. Bila ya shaka watasema ni Mwenyezi Mungu! Basi ni wapi wanakogeuziwa?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na ukiwauliza ni nani aliye waumba? Bila ya shaka watasema: Mwenyezi Mungu! Basi ni wapi wanako geuziwa? [87]

[87] Na ewe Mtume! Ukiwauliza hawa washirikina nani aliye waumba, bila ya shaka watasema: Kawaumba Mwenyezi Mungu. Basi inakuwaje wakaacha kumuabudu Mwenyezi Mungu Mtukufu wakenda kuwaabudu wenginewe, nao wanakiri kuwa Yeye ndiye Muumba wao? Ama hakika jambo hili ni la ajabu!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na ukiwauliza, ewe Mtume, hao washirikina wa watu wako, “Ni nani aliyewaumba?” watasema, «Allah Mtukufu Ndiye Aliyetuumba.» Basi vipi wao wanageuka na wanapotoka kwa kuacha kumuabudu Allah Mtukufu, Peke Yake, na kumshirikisha na asiyekuwa Yeye?

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Az-Zukhruf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net