Ruka hadi kwenye maudhui
Tafsir As-Saadi - Swahili · Az-Zukhruf
Sura ya 43

Az-Zukhruf

Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.

Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22

Aya ya 87

وَلَئِن سَأَلْتَهُم مَّنْ خَلَقَهُمْ لَيَقُولُنَّ ٱللَّهُ ۖ فَأَنَّىٰ يُؤْفَكُونَ 87

{87} Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: "Na ukiwauliza ni nani aliyewaumba. Bila ya shaka watasema ni Mwenyezi Mungu!" Yaani: Ukiwauliza washirikina kuhusu upweke wa Mwenyezi Mungu katika umola wake na nani Muumba, watakiri kuwa ni Mwenyezi Mungu peke yake, asiyekuwa na mshirika? "Basi ni wapi wanakogeuziwa?" Yaani: Vipi wanageuzwa mbali wakaacha kumwabudu Mwenyezi Mungu na kumkusudia Yeye peke yake? Kukiri kwao upweke wake katika umola, kunawalazimu kukiri upweke wake katika uungu, na hilo ni katika ushahidi mkubwa zaidi juu ya ubatili wa ushirikina.