Az-Zukhruf 43:86
الزخرفوَلَا يَمْلِكُ ٱلَّذِينَ يَدْعُونَ مِن دُونِهِ ٱلشَّفَـٰعَةَ إِلَّا مَن شَهِدَ بِٱلْحَقِّ وَهُمْ يَعْلَمُونَ
Wala hao mnaowaomba badala yake Yeye hawana uweza wa kumwombea mtu, isipokuwa anayeshuhudia kwa haki, na wao wanajua.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wala hao mnao waomba badala yake Yeye hawana uweza wa kumwombea mtu, isipo kuwa anaye shuhudia kwa haki, na wao wanajua. [86]
[86] Na hio miungu yao wanayo iabudu badala ya Mwenyezi Mungu haimiliki uweza wa kuwaombea hao wanao waabudu. Lakini wenye kushuhudia kwa Tawhidi, yaani hao wanao amini ya kwamba Mwenyezi Mungu ndiye Mola wao Mlezi kwa haki, hao wanaweza kuombewa miongoni mwa Waumini atakao Mwenyezi Mungu kuwaombea.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na hawamiliki, wale ambao washirikina wanawaabudu, uwezo wa kumuombea yoyote mbele ya Allah Mtukufu, isipokuwa wale waliyoishuhudia haki na wakakubali upweke wa Allah Mtukufu na unabii wa Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), na wakawa na yakini ya uhakika wa kile walichokikubali na kukitolea ushahidi.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net