Az-Zukhruf 43:85
الزخرفوَتَبَارَكَ ٱلَّذِى لَهُۥ مُلْكُ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا وَعِندَهُۥ عِلْمُ ٱلسَّاعَةِ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ
Na ametukuka Mwenye ufalme wa mbingu na ardhi na vilivyo kati yake. Na uko kwake ujuzi wa Saa ya Kiyama, na kwake Yeye mtarudishwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na ametukuka Mwenye ufalme wa mbingu na ardhi na viliomo ndani yake. Na uko kwake ujuzi wa Saa ya Kiyama, na kwake Yeye mtarudishwa. [85]
[85] Na ametukuka na ametaadhamu Yeye ambaye, peke yake, Mwenye ukamilifu wa kutekeleza katika mbingu na ardhi na baina yao katika viumbe vya angani vinavyo onekana na vyenginevyo, na mipango yote iko kwake, na Yeye tu ndiye Mwenye kujua wakati wa Kiyama, na kwake Yeye peke yake, mtarejeshwa mwishoe kwa ajili ya hisabu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Ni nyingi mno baraka za Allah Mtukufu na kheri Zake na ni mkubwa mno ufalme Wake, Ambaye ni Yake Peke Yake, mamlaka ya mbingu saba na ardhi saba na vitu vilivyoko baina yake, na Kwake Yeye Ndiko uliko ujuzi wa Wakati ambapo Kiyama kitasimama, na viumbe wafufuliwe kutoka makaburini mwao wapelekwe kwenye Kisimamo cha Hesabu, na Kwake Yeye mtarudishwa, enyi watu, baada ya kufa kwenu, na hapo alipwe kila mmoja kwa anayostahiki.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net