Az-Zukhruf 43:84
الزخرفوَهُوَ ٱلَّذِى فِى ٱلسَّمَآءِ إِلَـٰهٌ وَفِى ٱلْأَرْضِ إِلَـٰهٌ ۚ وَهُوَ ٱلْحَكِيمُ ٱلْعَلِيمُ
Na Yeye ndiye Mungu mbinguni, na ndiye Mungu katika ardhi. Naye ndiye Mwenye hekima, Mwenye kujua mno.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na Yeye ndiye Mungu mbinguni, na ndiye Mungu katika ardhi. Naye ndiye Mwenye hikima, Mwenye ujuzi. [84]
[84] Na Yeye ndiye anaye abudiwa mbinguni kwa haki, na anaabudiwa katika ardhi kwa haki. Na Yeye, peke yake, ndiye Mwenye hikima za mwisho katika vitendo vyake na mipango yake, Mwenye kujua kila kitu kilicho kuwa na kitakacho kuwa.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na Yeye Ndiye Allah Mtukufu, Peke Yake, Anayeabudiwa kwa haki, mbinguni na ardhini, na Yeye Ndiye Mwingi wa hekima Aliyeimarisha kuumba Kwake na kuitengeneza Sheria Yake, Mwenye ujuzi wa kila kitu kuhusu hali ya viumbe Vyake. Hakuna chochote kinachofichika katika hivyo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net