Az-Zukhruf 43:83
الزخرففَذَرْهُمْ يَخُوضُوا۟ وَيَلْعَبُوا۟ حَتَّىٰ يُلَـٰقُوا۟ يَوْمَهُمُ ٱلَّذِى يُوعَدُونَ
Basi waache wapige porojo wakicheza mpaka wakutwe na hiyo siku yao waliyoahidiwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Basi waache wapige porojo wakicheza mpaka wakutwe na hiyo siku yao waliyo ahidiwa. [83]
[83] Basi waachilie wazame katika upotovu wao, na wacheze katika dunia yao, wayaache mambo yenye maana, wala wasiyashughulikie, mpaka iwajie Siku ya Kiyama waliyo ahidiwa, ipate kila nafsi kulipwa kwa iliyo yachuma.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Basi waache, ewe Mtume, hao wenye kumzulia Allah Mtukufu urongo wazame kwenye ubatilifu wao, na wacheze katika dunia yao, mpaka wapambane na hiyo Siku yao ambayo wameahidiwa kuwa wataadhibiwa: ima hapa duniani au kesho Akhera au kote kuwili.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net