Az-Zukhruf 43:88
الزخرفوَقِيلِهِۦ يَـٰرَبِّ إِنَّ هَـٰٓؤُلَآءِ قَوْمٌ لَّا يُؤْمِنُونَ
Na usemi wake (Mtume) ni: ʻEwe Mola wangu Mlezi! Hakika hawa ni watu wasioamini.'
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na usemi wake (Mtume) ni: Ewe Mola wangu Mlezi! Hakika hawa ni watu wasio amini. [88]
[88] Naapa kwa kauli ya Muhammad s.a.w. anapo omba na kuita: Ewe Mola wangu Mlezi! Hakika hawa wenye inda ni watu wasio tarajiwa kuamini.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na Atasema, (rehema za Allah Mtukufu amani zimshukie), huku akishtakia watu wake waliomkanusha kwa Mola Wake kwa kusema, «Hawa watu hawakuamini wewe wala kile ulichonituma nacho kwao».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net