Az-Zukhruf 43:89
الزخرففَٱصْفَحْ عَنْهُمْ وَقُلْ سَلَـٰمٌ ۚ فَسَوْفَ يَعْلَمُونَ
Basi wasamehe, na uwaambie maneno ya salama. Watakujajua.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Basi wasamehe, na uwambie maneno ya salama. Watakuja jua. [89]
[89] Basi waachilie mbali, ewe Mtume, kwa wingi wa inda yao, na waambie: Langu mimi nikukuacheni kwa salama yenu kutoka kwangu, na salama yangu kutoka kwenu. Nanyi mtakuja jua kuwa mwisho wa inda yao ni khasara iliyo wazi.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Basi wasamehe, ewe Mtume, na uyapuuze maudhi yao, na lisitokee lolote kutoka kwako isipokuwa amani, ambalo ni neno linalosemwa na wenye akili na busara kuwaambia wajinga, kwani wao hawatukanani nao wala hawawalipizii kwa vitendo vyao vibaya walivyowafanyia. Basi watajua watakachokikuta cha balaa na adhabu. Hapa pana onyo na kitisho kikubwa kwa makafiri hawa wenye kushindana, na mfano wao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net