Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 43 · Aya ya 71

Az-Zukhruf 43:71

الزخرف

يُطَافُ عَلَيْهِم بِصِحَافٍ مِّن ذَهَبٍ وَأَكْوَابٍ ۖ وَفِيهَا مَا تَشْتَهِيهِ ٱلْأَنفُسُ وَتَلَذُّ ٱلْأَعْيُنُ ۖ وَأَنتُمْ فِيهَا خَـٰلِدُونَ

Maana

Watakuwa wanapitishiwa sahani za dhahabu na vikombe, na vitakuwemo ambavyo nafsi zinavipenda na macho yanavifurahia, na nyinyi mtakaa humo milele.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Watakuwa wanapitishiwa sahani za dhahabu na vikombe; na vitakuwamo ambavyo nafsi zinavipenda na macho yanavifurahia, na nyinyi mtakaa humo milele. [71]

[71] Na baada ya kuingia Peponi watakuwa wakizungukiwa kwa sahani za dhahabu, na bilauri kadhaalika, na humo watapata vyakula namna mbali mbali, na vinywaji vya kila namna. Na humo Peponi watapata kila kitamaniacho moyo, na kituzacho macho. Na kukamilisha furaha wataambiwa: Nyinyi mtakaa milele katika neema hizi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Watazungushiwa, hawa waliomuamini Allah Mtukufu na Mitume Wake, chakula ndani ya vyombo vya dhahabu na vinywaji ndani ya gilasi za dhahabu. Na humo watakuwa na kila ambacho nafsi zao zinakitamani na macho yao yanapendezwa nacho, na wao humo watakaa milele.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Az-Zukhruf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net