Az-Zukhruf 43:72
الزخرفوَتِلْكَ ٱلْجَنَّةُ ٱلَّتِىٓ أُورِثْتُمُوهَا بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ
Na hiyo ni Bustani ya mbinguni mliyorithishwa kwa mliyokuwa mkiyafanya.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na hiyo ni Pepo mliyo rithishwa kwa hayo mliyo kuwa mkiyafanya. [72]
[72] Na kutimiza neema, wataambiwa: Hii ndiyo Pepo mliyo ipata kwa sababu ya vitendo vyema mlivyo vitanguliza mlipo kuwa duniani.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na hii Pepo ambayo Allah Mtukufu Amewarithisha, ni kwa sababu ya kile mlichokuwa mkikifanya ulimwenguni cha mambo ya kheri na matendo mema, na akaifanya, kwa wema Wake na rehema Yake, ni malipo yenu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net