Az-Zukhruf 43:70
الزخرفٱدْخُلُوا۟ ٱلْجَنَّةَ أَنتُمْ وَأَزْوَٰجُكُمْ تُحْبَرُونَ
Ingieni Bustanini, nyinyi na wake zenu; mtafurahishwa humo.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Ingieni Peponi, nyinyi na wake zenu; mtafurahishwa humo. [70]
[70] Siku ya Kiyama wataambiwa kwa kufanyiwa hishima: Ingieni Peponi, nyinyi na wake zenu, nanyi mmo katika furaha iliyo kubwa, ambayo itadhihiri kwenye nyuso zenu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wataambiwa, «Ingieni Peponi, nyinyi na mfano wenu katika uchamungu, mkistareheshwa humo na mkifurahishwa».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net