Az-Zukhruf
Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.
Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22
يُطَافُ عَلَيْهِم بِصِحَافٍ مِّن ذَهَبٍ وَأَكْوَابٍ ۖ وَفِيهَا مَا تَشْتَهِيهِ ٱلْأَنفُسُ وَتَلَذُّ ٱلْأَعْيُنُ ۖ وَأَنتُمْ فِيهَا خَـٰلِدُونَ 71
{71} "Watakuwa wanapitishiwa sahani za dhahabu na vikombe" bora zaidi wakihudumiwa na wavulana wa ujana wa milele. "Na vitakuwemo ambavyo nafsi zinavipenda na macho yanavifurahia" kama vile vyakula, vinywaji, mavazi, ndoa, na kile kinachopendeza macho kama vile mandhari mazuri, miti ya mabustanini, neema nzuri sana na majengo yaliyopambwa. Hivyo vyote vimeandaliwa humo kwa ajili ya watu wake kwa njia kamili na bora zaidi. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Watapata humo kila namna ya matunda na watapata kila watakachokitaka." Na akasema: "Na nyinyi mtakaa humo milele. " Hiki ndicho cha kukamilisha neema ya wale walioko Peponi. Nayo inajumuisha kuendelea daima kwa neema yake, kuongezeka kwake, na kutokatika kwake.