Az-Zukhruf 43:52
الزخرفأَمْ أَنَا۠ خَيْرٌ مِّنْ هَـٰذَا ٱلَّذِى هُوَ مَهِينٌ وَلَا يَكَادُ يُبِينُ
Au mimi si bora kuliko huyu aliye mnyonge, wala hawezi kusema waziwazi?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Au mimi si bora kuliko huyu aliye mnyonge, wala hawezi kusema waziwazi? [52]
[52] Firauni akasema akizidisha ujabari: Bali mimi ni bora kuliko dhaifu huyu mnnyonge, asiye weza hata kubainisha wazi huo wito wake kwa ulimi wa fasaha.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Bali mimi ni bora kuliko huyu asiye na utukufu. Kwani yeye anajidhalilisha katika kutaka matakwa yake yatimie kwa udhaifu wake na unyonge, na hafafanui maneno kwa ajili ya uzito wa ulimi wake. Na lililomfanya Fir’awn atoe kauli hii ni ukafiri, ushindani na uzuiaji njia ya Allah Mtukufu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net