Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 43 · Aya ya 51

Az-Zukhruf 43:51

الزخرف

وَنَادَىٰ فِرْعَوْنُ فِى قَوْمِهِۦ قَالَ يَـٰقَوْمِ أَلَيْسَ لِى مُلْكُ مِصْرَ وَهَـٰذِهِ ٱلْأَنْهَـٰرُ تَجْرِى مِن تَحْتِىٓ ۖ أَفَلَا تُبْصِرُونَ

Maana

Na Firauni alitangaza kwa watu wake akisema: 'Enyi watu wangu! Kwani mimi si ninao huu ufalme wa Misri, na hii mito inapita chini yangu. Je, hamwoni?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na Firauni alitangaza kwa watu wake, akisema: Enyi watu wangu! Kwani mimi sinao huu ufalme wa Misri, na hii mito inapita chini yangu? Je! Hamwoni? [51]

[51] Firauni akawatangazia watu wake kutangaza nguvu zake na madaraka yake: Kwani huu ufalme wa Misri si wangu mimi peke yangu, wala hapana mwenginewe, na hii mito ambayo mnaiona inapita chini ya jumba langu? Hamyaoni haya? Basi hamzingatii mnayo yaona ya nguvu zangu na udhaifu wa Musa? Na Firauni alitaka kwa wito wake kuutia imara ut'iifu wao.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na Fir’awn aliita mbele ya wakubwa wa watu wake kwa kujigamba na kujisifu kwa ufalme wa Misri, «Je, kwani mimi sina ufalme wa Misri na mito hii inayopita chini yangu? Kwani hamuoni utukufu wangu na nguvu zangu na unyonge wa Mûsã na umasikini wake?».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Az-Zukhruf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net