Az-Zukhruf 43:53
الزخرففَلَوْلَآ أُلْقِىَ عَلَيْهِ أَسْوِرَةٌ مِّن ذَهَبٍ أَوْ جَآءَ مَعَهُ ٱلْمَلَـٰٓئِكَةُ مُقْتَرِنِينَ
Basi mbona hakuvikwa vikuku vya dhahabu au hawakuja Malaika pamoja naye wakamwandama?'
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Basi mbona hakuvikwa vikuku vya dhahabu, au hawakuja Malaika pamoja naye wakamwandama? [53]
[53] Akazidi kusema kuchochea kumkadhibisha Musa: Lau ingeli kuwa Mola wake Mlezi angeli mvika vikuku vya dhahabu kwa kumpa funguo za utawala, au akamsaidia kwa Malaika wa kumuunga mkono, ingeli kuwa yeye ni mkweli katika madai yake ya Utume?
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Basi si apewe huyo Mûsã, iwapo ni mkweli kuwa yeye ni Mjumbe wa Mola wa viumbe wote, vidani vya dhahabu, au waje Malaika pamoja naye wameshikana na kukutana na wakafuatana wakimtolea ushahidi kuwa yeye ni Mtume wa Allah Mtukufu kwetu sisi.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net