Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 43 · Aya ya 54

Az-Zukhruf 43:54

الزخرف

فَٱسْتَخَفَّ قَوْمَهُۥ فَأَطَاعُوهُ ۚ إِنَّهُمْ كَانُوا۟ قَوْمًا فَـٰسِقِينَ

Maana

Basi aliwachezea watu wake na wakamtii. Kwa hakika hao walikuwa watu wapotovu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Basi aliwachezea watu wake, na wakamt'ii. Kwa hakika hao walikuwa watu wapotovu. [54]

[54] Firauni akawa anawachochea watu wake, na akawaathiri kwa udanganyifu huu, nao wakamt'ii katika upotovu wake. Kwani hao walikuwa watu walio kwisha toka kwenye Dini ya Mwenyezi Mungu Iliyo Nyooka.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Fir’awn akazichezea akili za watu wake, akawaita kwenye upotevu na wao wakamtii na wakamkanusha Mûsã. Kwa hakika, wao walikuwa ni watu waliotoka kwenye utiifu wa Allah Mtukufu na njia yake ya sawa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Az-Zukhruf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net