Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 43 · Aya ya 55

Az-Zukhruf 43:55

الزخرف

فَلَمَّآ ءَاسَفُونَا ٱنتَقَمْنَا مِنْهُمْ فَأَغْرَقْنَـٰهُمْ أَجْمَعِينَ

Maana

Walipotukasirisha, tuliwapatiliza tukawazamisha wote!

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Walipo tukasirisha tuliwapatiliza tukawazamisha wote! [55]

[55] Basi walipo tughadhibisha hadi ya kutughadhibisha, kwa kupita kwao mipaka ya ufisadi, tuliwaangamiza kwa kuwazamisha wote.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Walipotukasirisha, kwa kutuasi na kumkanusha Mûsã na miujiza aliyokuja nayo, tuliwatesa kwa adhabu ya duniani tuliyowaharakishia na tukawazamisha wote baharini.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Az-Zukhruf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net