Az-Zukhruf 43:45
الزخرفوَسْـَٔلْ مَنْ أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ مِن رُّسُلِنَآ أَجَعَلْنَا مِن دُونِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ءَالِهَةً يُعْبَدُونَ
Na waulize Mitume wetu tuliowatuma kabla yako: 'Je, tulifanya miungu mingine iabudiwe badala ya Rahmani?'
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na waulize Mitume wetu tulio watuma kabla yako: Je! Tulifanya miungu mingine iabudiwe badala ya Rah'mani? [45]
[45] Na hebu angalia katika sharia za Mitume wetu tulio watuma kabla yako. Ati umekuja humo wito wa kuwaita watu wende kuabudu vitu visio kuwa Mwenyezi Mungu? Haukuja! Basi hao wanao abudu asiye kuwa Mwenyezi Mungu mmoja hadi wamepita mipaka katika upotovu wao!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na uwaulize, ewe Mtume, wafuasi wa wale tuliowatuma kabla yako miongoni mwa Mitume wetu na wabebaji sheria zao, «Je walikuja Mitume wao na ujumbe wa kuabudiwa asiyekuwa Allah Mtukufu? Wao watakupasha habari kuwa hilo halikutokea, kwani Mitume wote walilingania kile ulichowaitia watu cha kumuabudu Allah Mtukufu, Peke Yake Asiye na mshirika, na wakakataza kuabudiwa asiyekuwa Allah Mtukufu».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net