Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 43 · Aya ya 46

Az-Zukhruf 43:46

الزخرف

وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا مُوسَىٰ بِـَٔايَـٰتِنَآ إِلَىٰ فِرْعَوْنَ وَمَلَإِي۟هِۦ فَقَالَ إِنِّى رَسُولُ رَبِّ ٱلْعَـٰلَمِينَ

Maana

Na bila ya shaka tulimtuma Musa kwa Ishara zetu aende kwa Firauni na waheshimiwa wake, na akasema: 'Hakika mimi ni Mtume wa Mola Mlezi wa walimwengu wote!'

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na bila ya shaka tulimtuma Musa kwa Ishara zetu ende kwa Firauni na waheshimiwa wake, na akasema: Hakika mimi ni Mtume wa Mola Mlezi wa walimwengu wote! [46]

[46] Na bila ya shaka Sisi tulimtuma Musa tukampa miujiza yenye kuthibitisha ukweli wake, ende kwa Firauni na watu wake. Akasema: Hakika mimi ni Mtume wa Muumba wa walimwengu wote na Mlezi wao nimetumwa kwenu. Wakamtaka aonyeshe miujiza.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na kwa hakika tulimtuma Mûsã kwa hoja zetu aende kwa Fir’awn na wakubwa wa watu wake kama tulivyokutuma wewe, ewe mtume, kwa hawa washirikina wa watu wako, na Mûsã akawaambia, «Mimi ni Mtume kutoka kwa Mola wa viumbe wote».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Az-Zukhruf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net