Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 43 · Aya ya 47

Az-Zukhruf 43:47

الزخرف

فَلَمَّا جَآءَهُم بِـَٔايَـٰتِنَآ إِذَا هُم مِّنْهَا يَضْحَكُونَ

Maana

Lakini alipowajia na Ishara zetu, wakaingia kuzicheka.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Lakini alipo wajia na Ishara zetu wakaingia kuzicheka. [47]

[47] Alipo wajia kwa miujiza ya kuthibitisha Utume wake mara wakampokea kwa kumcheka, na kumfanyia tashtiti, na kumcheza shere, bila ya kuzingatia maneno yake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na alipowajia na dalili zilizo wazi zenye kuonyesha ukweli wake katika ulinganizi wake, hapo Fir’awn na viongozi wa utawala wake wakawa wanazicheka zile hoja na mazingatio aliyokuja nayo Mûsã.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Az-Zukhruf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net