Az-Zukhruf 43:48
الزخرفوَمَا نُرِيهِم مِّنْ ءَايَةٍ إِلَّا هِىَ أَكْبَرُ مِنْ أُخْتِهَا ۖ وَأَخَذْنَـٰهُم بِٱلْعَذَابِ لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ
Na hatukuwaonyesha Ishara yoyote ila hiyo ilikuwa kubwa zaidi kuliko nyingineye. Na tukawakamata kwa adhabu ili warejee.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na hatukuwaonyesha Ishara yoyote ila hiyo ilikuwa kubwa zaidi kuliko nyenginewe. Na tukawakamata kwa adhabu ili warejee. [48]
[48] Na kila muujiza katika miujiza iliyo wajia mfululizo, kwa uwazi wa hoja zake juu ya ukweli wa Mtume, na kuwa kila mmoja peke yake unatimiza makusudio hayo kwa ukamilifu wa kila njia, na ukamilifu wa nafsi yake, hata ukiuangalia waweza kusema: Muujiza huu ni mkubwa kuliko ule mwengine. Na walipo shikilia kuendelea na uasi tuliwapatiliza kwa balaa za namna kwa namna, ili warejee, waache upotovu wao.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na hatukuwa tukimuonyesha Fir’awn hoja yoyote isipokuwa huwa ni kubwa zaidi kuliko ile iliyokuwa kabla yake, na inautolea dalili zaidi usahihi wa kile ambacho Mûsã alikuwa akiwalingania kwacho. Na tuliwapatiliza kwa aina mbalimbali za adhabu, kama vile Nzige, chawa, vyura, mafuriko na nyinginezo, ili wapate kurudi kwenye kumpwekesha Allah Mtukufu na kumtii na kuacha kumkanusha .
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net