Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 43 · Aya ya 49

Az-Zukhruf 43:49

الزخرف

وَقَالُوا۟ يَـٰٓأَيُّهَ ٱلسَّاحِرُ ٱدْعُ لَنَا رَبَّكَ بِمَا عَهِدَ عِندَكَ إِنَّنَا لَمُهْتَدُونَ

Maana

Na wakasema: 'Ewe mchawi! Tuombee kwa Mola wako Mlezi kwa ile ahadi aliyokuahidi; hakika sisi tutakuwa wenye kuongoka.'

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wakasema: Ewe mchawi! Tuombee kwa Mola wako Mlezi kwa ile ahadi aliyo kuahidi; hakika sisi tutakuwa wenye kuongoka. [49]

[49] Wakasema, kumlilia Musa balaa zilipo waenea: Ewe mchawi - ndio Mwanachuoni kikwao - Tuombee kwa Mola wako Mlezi, kwa kutawasali na ahadi yake aliyo kupa, atuondolee adhabu hii! Hakika sisi tukifarijiwa bila ya shaka tutaongoka.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na Fir’awn na viongozi wa utawala wake wakasema kumwambia Mûsã, “Ewe mjuzi! (Na mchawi alikuwa kwao ni mtu mkubwa wanayemheshimu, na haukuwa uchawi ni sifa ya mtu kutukanika), Tuombee kwa mola wako, kwa ile ahadi Aliyokuahidi na yale matukufu Aliyokutunukia wewe mahsusi, Atuepushie adhabu, kwani tukiepushiwa adhabu, kwa hakika sisi ni wenye kuongoka na kuayaamini yale uliyotujia nayo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Az-Zukhruf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net