Az-Zukhruf 43:44
الزخرفوَإِنَّهُۥ لَذِكْرٌ لَّكَ وَلِقَوْمِكَ ۖ وَسَوْفَ تُسْـَٔلُونَ
Na hakika haya ni ukumbusho kwako na kwa kaumu yako. Na mtakuja ulizwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na hakika haya ni ukumbusho kwako na kwa kaumu yako. Na mtakuja ulizwa. [44]
[44] Na hakika hii Qur'ani ni utukufu mkubwa juu yako, ewe Muhammad, na wa Umma wako, kwa kuwa umeteremshiwa kwa lugha ya Kiarabu, na mtakuja kuhojiwa Siku ya Kiyama juu ya haki yake, na shukrani za neema zake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na hii Qur’ani ni utukufu na ukumbusho kwako na kwa watu wako miongoni mwa washirikina wa kikureishi (na wengineo), kwa kuwa imeteremshwa kwa lugha yao, kwa kuwa wao wanaifahamu zaidi kuliko watu wengine, na kwa hivyo inatakiwa wawe ni watu wenye kusimama nayo zaidi, na ni wenye kufanya matendo yanayoambatana nayo zaidi. Na mtaulizwa, wewe na walio pamoja na wewe, kuhusu vile mlivyoshukuru kuletewa hiyo Qur’ani na mlivyoifanyia kazi.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net