Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 43 · Aya ya 36

Az-Zukhruf 43:36

الزخرف

وَمَن يَعْشُ عَن ذِكْرِ ٱلرَّحْمَـٰنِ نُقَيِّضْ لَهُۥ شَيْطَـٰنًا فَهُوَ لَهُۥ قَرِينٌ

Maana

Anayeyafanyia upofu maneno ya Rahmani tunamwekea Shetani kuwa ndiye rafiki yake.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Anaye yafanyia upofu maneno ya Rahmani tunamwekea Shet'ani kuwa ndiye rafiki yake. [36]

[36] Na mwenye kujitia upofu na Qur'ani aliyo iteremsha Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema kuwa ni kumbusho kwa walimwengu wote, tunamsalitisha na Shetani, anakuwa naye daima, akimpoteza na akimzuzua.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na mwenye kuupa mgongo utajo wa Mwingi wa Rehema, nao ni Qur’ani, asiogope mateso yaliyotajwa ndani yake na asijiongoze kwa uongofu wake, tutamwekea Shetani hapa duniani wa kumpoteza, ikiwa ni malipo yake ya kuupa mgongo kwake utajo wa Allah Mtukufu. Shetani huyo atakuwa na yeye wakati wote na kufuatana naye, akimkataza ya halali na kumsukuma afanye ya haramu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Az-Zukhruf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net